Isaiah 49:17-23

17 aWana wako wanaharakisha kurudi,
nao wale waliokuteka wanaondoka kwako.
18 bInua macho yako ukatazame pande zote:
wana wako wote wanakusanyika na kukujia.
Kwa hakika kama vile niishivyo,
utawavaa wote kama mapambo,
na kujifunga nao kama bibi arusi,”
asema Bwana.

19 c“Ingawa uliangamizwa na kufanywa ukiwa,
na nchi yako ikaharibiwa,
sasa nafasi itakuwa finyu kwa ajili ya watu wako,
nao wale waliokuangamiza watakuwa mbali sana.
20 dWatoto waliozaliwa wakati wa msiba wako
bado watakuambia,
‘Mahali hapa ni finyu sana kwetu,
tupe eneo kubwa zaidi la kuishi.’
21 eNdipo utasema moyoni mwako,
‘Ni nani aliyenizalia hawa?
Nilikuwa nimefiwa, tena tasa;
nilikuwa nimehamishwa na kukataliwa.
Ni nani aliyewalea hawa?
Niliachwa peke yangu,
lakini hawa wametoka wapi?’ ”
22 fHili ndilo asemalo Bwana Mwenyezi:

“Tazama, nitawaashiria watu wa Mataifa,
nitainua bendera yangu kwa mataifa;
watawaleta wana wako mikononi yao,
na kuwabeba binti zenu juu ya mabega yao.
23Wafalme watakuwa baba zenu wa kuwalea,
na malkia wao watakuwa mama zenu wa kuwalea.
Watasujudu mbele yako nyuso zao zikigusa ardhi;
wataramba mavumbi yaliyo miguuni mwako.
Ndipo utajua ya kuwa Mimi ndimi Bwana;
wale wanaonitumaini mimi hawataaibika.”
Copyright information for SwhNEN